
Mathayo 5:3-10
'Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni, maana watafarijiwa. Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema, maana hao wataonyeshwa rehema. Heri walio safi moyoni, maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.'
