Mathayo 3:1-3
Siku zile alikuja Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, akisema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Mtengenezeni Bwana njia, mnyoshee mapito yake.